Taasisi 8 za haki za binadamu zimewataka maafisa wa Lebanon
kuacha kuwarejesha wakimbizi wa Palestina wanaokimbia mgogoro wa Syria.
Taasisi hizo zikiwemo Kituo cha Haki za Binadamu cha Lebanon, Taasisi ya
Haki za Binadamu ya Palestina na Mtandano wa Haki za Bindamu wa Ulaya
na Mediterranean zimesema kuwa, katika hali ambayo ni rahisi kwa Wasyria
wanaokimbia machafuko kuingia Lebanon, kumeripotiwa matukio kadhaa ya
kuwazuia wakimbizi wa Palestina wanaokimbia vita Syria kuingia na kupata
hifadhi nchini Lebanon.
Taasisi hizo zimeashiria kufukuzwa nchini Lebanon wakimbizi wa
Palestina wanaotokea Syria mwezi huu wa Mei na kusema kuwa hatua hiyo ni
kinyume na Mkataba wa Umoja wa Mataifa unaopinga mateso. Maafisa wa
Lebanon wametakiwa na taasisi hizo za kutetea haki za binadamu kuwapa
haki wanazostahili wakimbizi wa Palestina wanaotokea Syria sawa na
wanavyofanya kwa wakimbizi wa Syria.
No comments:
Post a Comment