Serikali ya Somalia imeitaka serikali ya Ethiopia iisaidie kuwalinda
wanadiplomasia wa kigeni pamoja na wafanyakazi wa mashirika ya misaada
ya kibinadamu. Buri Muhammad Hamza, Mshauri Mkuu wa Rais wa Somalia
ametoa ombi hilo alipokutana na kufanya mazungumzo na Wondimu Asamnenu
balozi wa Ethiopia mjini Mogadishu na kusisitiza kwamba, wanaitaka
serikali ya Addis Ababa ishiriki katika kudhamini ulinzi na usalama wa
wafanyakazi wa mashirika ya utoaji misaada ya kibinaadamu pamoja na
wanadiplomasia wa kigeni walioko nchini humo.
Aidha Buri Hamza amesema
katika mazungumzo yake na balozi huyo wa Ethiopia kwamba, hadi sasa
Addis Ababa imekuwa mwenyeji wa mikutano kadhaa ya amani na usalama
nchini Somalia na vile vile kuna maelfu ya Wasomalia waliokimbia nchini
Ethiopia na kuomba hifadhi huko kutokana na nchi yao kukabiliwa na
machafuko. Mshauri Mkuu wa Rais wa Somalia ambaye pia ni msemaji wa Rais
ameongeza kuwa, wanajeshi wa Ethiopia wanashirikiana na vikosi vya
kulinda amani vya Umoja wa Afrika AMISOM katika kupambana na wanamgambo
wa al-Shabab hali inayoonesha kuweko ushirikiano mzuri kati ya Mogadishu
na Addis Ababa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment