Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, wameitaka Serikali ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ),
kuzipatia ufumbuzi kero za Muungano, ambazo baadhi yake zimekuwa
zikirudisha nyuma maendeleo ya wananchi na kukwamisha juhudi za
kupambana na umasikini. Kauli hiyo imetolewa na Mwenyeviti wa Wenyeviti
wa Baraza la Wawakilishi, Hamza Hassan Juma, wakati akisoma taarifa ya
kamati yake pamoja na kuchangia Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha
2014-2015 katika Baraza la Wawakilishi.
Hamza Hassan Juma amesema kuwa,
wananchi wamekuwa wakisikitishwa na kuwepo kwa vikwazo vya biashara
katika maeneo ya Tanzania Bara na Zanzibar na hivyo kurudisha nyuma
shughuli zao za kibiashara, usafirishaji wa mizigo na uingizaji. Baadhi
ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wamezitaka serikali zote mbili
kuharakisha kuondosha usumbufu wa wafanyabiashara katika kuingiza bidhaa
mbalimbali katika Bandari ya Dar es Salaam na Malindi iliyopo Unguja.
Inaelezwa kuwa, wafanyabiashara wadogo, wakiwemo wanawake, wamevunjika
moyo na wengine kuacha kufanya shughuli za kibiashara, kwa sababu ya
vikwazo vya ushuru mkubwa kwa watendaji wa kodi za mapato.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment