Mazungumzo ya amani ya Sudan Kusini yamesogezwa mbele na sasa
yatafanyika mwezi ujao wa Juni. Mtandao wa Habari wa al-Yaums Sabi'i
umeinukuu ya Jumuiya ya kieneo ya Mashariki mwa Afrika IGAD Iikitangaza
kwamba, pande mbili hasimu huko Sudan Kusini zitakutana tena katika
mazungumzo ya amani tarehe 4 ya mwezi ujao wa Juni.
Taarifa ya IGAD imebainisha kwamba, imezitaka pande zinazozozan huko
Sudan Kusini kuunda kamati mbili za kisiasa na kiusalama.
Aidha Jumuiya
ya kieneo ya Mashariki mwa Afrika IGAD imesisitiza juu ya udharura wa
kuheshimiwa makubaliano ya usitishaji vita nchini Sudan Kusini.
Kufuatia mashinikizo ya kimataifa vikosi vya serikali ya Rais Salva
Kiir wa Sudan Kusini na wanamgambo watiifu kwa kiongozi wa waasi Riek
Machar hivi karibuni walilazimika kutia saini makubaliano ya amani mjini
Addis Abbas Ethiopia, lakini bado vipengee vya makubaliano hayo
havijatekelezwa ipasavyo.
No comments:
Post a Comment