Duru za Lebanon zimearifu kwamba, nchi za Saudia, Qatar na Uturuki
zimeendelea kushirikiana kijeshi na kitaarifa na magaidi wanaopigana
dhidi ya serikali ya Rais Bashar al-Assad wa Syria. Ripoti hizo
zinabainisha kwamba, idadi kadhaa ya maafisa wa kiusalama wa Saudi
Arabia, Qatar na Uturuki wamekuwa wakishirikiana kikamilifu na magaidi
huko Syria.
Gazeti la Lebanon la al-Jamhuriyah limefichua kwamba, hata
kuna maafisa wa ngazi za juu wa kijeshi wa Saudia, Qatar na Uturuki
ambao wako nchini Syria. Aidha gazeti hilo linabainisha zaidi kwamba,
miongoni mwa magaidi waliouawa nchini Syria kuna maafisa wa kiusalama wa
Saudia na Qatar na kwamba, hivi sasa Riyadh na Doha zinafanya juhudi za
kurejeshwa viwiliwili hivyo ili vikazikwe katika nchi zao. Machafuko
nchini Syria yalianza mwaka 2011 na serikali ya Damascus inazilaumu nchi
za Magharibi zikiongozwa na Marekani, Uingereza na Ufaransa pamoja na
waitifaki katika eneo yaani Saudi Arabia, Uturuki, Qatar na utawala wa
Kizayuni wa Israel, kuwa ndio waungaji mkono wakuu wa magaidi wanaotaka
kuiangusha serikali halali ya Rais Bashar Assad na ambao hadi sasa
wametenda jinai kubwa dhidi ya raia wa nchi hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment