Mkuu wa Vikosi vya Anga vya Libya ametangaza kuwa anamuunga mkono
jenerali mstaafu Khalifa Haftar katika operesheni zake za kupambana na
makundi yenye silaha katika mji wa Benghazi. Mkuu wa vikosi vya anga vya
Libya pia amewataka wananchi kuuunga mkono jeshi la Haftar linaloitwa
'Jeshi la Taifa la Libya'. Haftar pia ameungwa mkono na Idara ya
Upelelezi ya Kijeshi ya Libya.
Hayo yanajiri huku jeshi la Marekani likijitayarisha kuwaondoa raia
wake katika ubalozi wa nchi hiyo mjini Tripoli na serikali ya mpito ya
Libya kutangaza tarehe ya uchaguzi wa Bunge.
Machafuko yalishtadi Libya
siku ya Ijumaa baada ya jenerali mstaafu Khalifa Haftar kuanzisha
mashambulio ya anga na nchi kavu dhidi ya makundi ya wanamganbo katika
mji wa Benghazi, ambayo baadhi yanaunga mkono serikali ya mpito ya
Tripoli. Haftar ameapa kuwa hatoacha mashambulizi hayo hadi makundi
yaliyofurutu ada yatakaposambaratika.
No comments:
Post a Comment