Marekani imesema kuwa itaiadhibu
Russia kwa kuiwekea vikwazo zaidi iwapo Moscow na washirika wake
watavuruga uchaguzi ujao wa rais nchini Ukraine. John Kerry, Waziri wa
Mambo ya Nje wa Marekani amesema katika mazungumzo na wenzake wa Ulaya
kwamba, wananchi wa Ukraine wanapaswa kuachwa wajiamulie mustakbali wao
na kwamba iwapo Russia au washirika wake watavuruga uchaguzi huo
watawekewa vikwazo vya kiuchumi.
Serikali ya mpito ya Ukarine imepanga
kufanya uchaguzi wa rais Mei 25 huku wasiwasi ukiongezeka katika maeneo
ya mashariki mwa nchi hiyo yanayotaka kujitenga.
Marekani na nchi za Ulaya zinaituhumu
Russia kuwa inachochea machafuko nchini Ukraine hatua inayopelekea
baadhi ya maeneo yatake kujitenga.
No comments:
Post a Comment