Mahakama moja nchini Morocco imewahukumu kifungo jela wanachama 26 wa
kundi moja la kitakfiri kwa tuhuma za kutuma wapiganaji katika sehemu
mbalimbali za eneo la Sahel la Afrika kwa ajili ya kufanya mauji na
vitendo vya kikatili. Mahakama hiyo imemuhukumu Mustapha Kadawi,
kiongozi wa kundi hilo kifungo cha miaka 20 jela na kulipa faini ya
kiasi cha Euro elfu 50. Mustapha anatajwa kuhusika katika kuunda na
kuandaa mashambulizi ya kigaidi, kuunga mkono kifedha harakati za
kigaidi, kuwashawishi wapiganaji wake kufanya vitendo hivyo, kuwa
mwanachama wa kundi la kitakfiri lililopigwa marufuku nchini humo na
kuitisha vikao mbalimbali bila kibali cha serikali.
Kwa mujibu wa ripoti
hiyo watu wengine 25 katika kesi hiyo wamehukumiwa vifungo vya miaka
miwili hadi mitano na Mahakam hiyo. Morocco ilipiga marufuku ya makundi
yenye misimamo ya kufurutu ada yapatayo 100, kufuatia miripuko ya mwaka
jana katika mji wa Darul Baidha nchini humo. Hivi karibuni pia, serikali
ya Rabat ilionyesha masikitiko yake kutokana na kuwepo baadhi ya
harakati za kitakfiri zinazojihusisha na utumaji nchini Syria wapiganaji
ambao baadaye hujiunga na makundi ya kigaidi kwa lengo la kutaka
kuiangusha serikali halali ya Rais Bashar al-Assad wa nchi hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment