Sergei Lavrov Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Russia amesema kuwa,
migogoro mingi inayojitokeza katika nchi mbalimbali duniani husababishwa
na juhudi za kutaka kuziondosha kimabavu na kinyume cha sheria serikali
zilizoko madarakani. Lavrov ameongeza kuwa, migogoro yote
iliyoshuhudiwa katika nchi za Syria, Libya, Iraq na hali kadhalika
Ukraine, inatokana na kuwepo njama za kuzibadilisha serikali zilizoko
madarakani kinyume cha sheria. Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Russia
amesisitiza kuwa, kuna ulazima wa kuanzishwa mkakati wa kukomeshwa
ukandamizaji na machafuko na kushirikisha makundi yote bila ya masharti
yoyote.
Siku ya Jumatano iliyopita, Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa
Russia alionya juu ya kutokea 'vita vya kindugu' nchini Ukraine. Lavrov
alimtuhumu John Kerry Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Marekani na
viongozi wengine wa nchi za Ulaya kwa kusababisha mgogoro wa Ukraine.
Lavrov amezitaka pande mbili zinazopigana nchini Ukraine kuketi kwenye
meza ya mazungumzo ya amani, kwa lengo la kukomesha machafuko nchini
humo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment