Mkuu wa Kamisheni ya Usalama wa Taifa na Sera za Kigeni ya Jamhuri ya
Kiislamu ya Iran amesema kuwa, jiji la Tehran kuanzia kesho litakuwa
mwenyeji wa kikao cha pili cha Wakuu wa Kamisheni za Usalama wa Taifa
kutoka nchi marafiki wa Syria. Alauddin Bourujerdi ameongeza kuwa,
wajumbe kutoka nchi zisizopungua 25 watashiriki kwenye kikao hicho.
Bourujerdi ameongeza kuwa, vikao hivyo vinafanyika kwa shabaha ya
kusaidia kukomesha mapigano nchini Syria sanjari na kuyapa nguvu
mapambano ya muqawama dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel.
Mkuu wa
Kamisheni ya Usalama wa Taifa na Sera za Kigeni wa Iran amesisitiza
kwamba kuna ulazima wa kuendelezwa zoezi la upelekaji misaada ya
kibinadamu kwa wananchi wa Syria ikiwemo chakula na madawa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment