Kiongozi wa waasi wa Sudan
Kusini na Makamu wa zamani wa Rais wa nchi hiyo Riek Machar amesema ana
nia ya kweli ya kutaka amani na yuko tayari kuendelea na mazungumzo juu
ya suala hilo. Katika taarifa aliyotoa mjini Nairobi, Kenya hapo jana,
kufuatia mazungumzo yake na Rais Uhuru Kenyatta wa nchi hiyo, Machar
amesema na hapa ninamnukuu:"Nimekuja kusukuma mbele mchakato huu; na
ninataka nikuhakikishieni kwamba tuna nia ya dhati kuhusu kuleta amani
Sudan Kusini", mwisho wa kumnukuu.
Duru ijayo ya mazungumzo kati ya
serikali ya Sudan Kusini na waasi wanaopigana na jeshi la serikali hiyo
imepangwa kufanyika tarehe 4 ya mwezi ujao wa Juni huko mjini Addis
Ababa, Ethiopia.
Wakati huohuo imeelezwa kuwa
Jumuiya ya Kieneo ya nchi za Afrika Mashariki IGAD itatuma kikosi cha
kusimamia makubaliano ya usitishaji vita huko Sudan Kusini. Mwakilishi
wa IGAD nchiniSudan Kusini Jenerali Lazaro Sumbeiywo amesema kikosi
hicho kitatumwa nchini humo mwezi ujao wa Juni kwa madhumuni ya
kusimamia utekelezaji mzuri wa makubaliano ya usitishaji mapigano kati
ya vikosi vya serikali na vile vya waasi. Amesema nchi zinazotarajiwa i
kuchangia askari wa kikosi hicho ni Ethiopia, Djibouti, Kenya, Rwanda na
Burundi
No comments:
Post a Comment