Rais John Dramani Mahama wa Ghana amesema Jumuiya ya Uchumi ya Nchi za
Magharibi mwa Afrika ECOWAS itatekeleza jukumu lake kuhusiana na
migogoro katika nchi za Nigeria na Mali. Rais wa Ghana amesisitiza
kwamba nchi za Magharibi mwa Afrika hazitoruhusu maendeleo yaliyoletwa
na wananchi wa nchi hizo yavurugwe kutokana na hatua za ubinafsi za
baadhi ya makundi.
Akizungumza baada ya kikao cha dharura cha ECOWAS
kilichofanyika jana usiku katika mji mkuu wa Ghana Accra, Dramani Mahana
ambaye ni mwenyekiti wa sasa wa jumuiya hiyo amesema nchi wanachama wa
ECOWAS hazitoungojea Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kukabiliana na
kupambana na migogoro na machafuko. Rais wa Ghana amebainisha kuwa nchi
za Kiafrika zinakabiliwa na aina mpya ya vitisho na kwamba tishio dhidi
ya nchi yoyote ya bara hilo linahesabiwa kuwa tishio kwa nchi zote za
Magharibi mwa Afrika. Hali si shwari nchini Nigeria baada ya wanafunzi
wa kike zaidi ya 200 wa shule ya Chibok iliyoko katika jimbo la Borno
kaskazini mashariki mwa nchi hiyo kutekwa nyara na kundi la Boko Haram
mwezi uliopita wa Aprili. Huko kaskazini mwa Mali pia kunashuhudiwa
wimbi jipya la machafuko lililoanzishwa na wapinzani wa serikali
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment