Naibu Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran anayeshughulikia masuala ya
nchi za Kiarabu na Kiafrika amesema kuwa, Tehran iko tayari kuisaidia
Nigeria katika kuipatia ufumbuzi kadhia ya kutekwa nyara wanafunzi wa
kike zaidi ya 200. Hossein Amir-Abdollahian amesema hayo katika
mazungumzo yake na Tukur Mani, balozi wa Nigeria hapa mjini Tehran na
kusisitiza kwamba, serikali ya Iran inatangaza utayarifu wake wa
kuisaidia Nigeria katika kuwakomboa wasichana hao wanaoshikiliwa na
kundi la Kitakfiri la Boko Haram.
Kwa upande wake Tukur Mani, balozi wa
Nigeria hapa mjini Tehran ameishukuru serikali ya Iran kwa kuwa pamoja
na serikali na taifa la Nigeria sambamba na hatua ya Tehran ya kulaani
vitendo vya kigaidi. Wakati huo huo, Hamid Reza Dehqani, Mwakilishi wa
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu
OIC amezitaka nchi za Kiislamu kukabiliana na makundi ya kitakfiri kama
lile la Boko Haram la nchini Nigeria. Wanafunzi hao wa kike walitekwa
nyara na kundi la Boko Haram tarehe 14 ya mwezi uliopita katika shule
moja ya sekondari iliyoko katika mji wa Chobok kwenye jimbo la Borno.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment