George Galloway, mbunge mashuhuri wa bunge la Uingereza amesema Abdel
Fattah el Sisi, mgombea urais wa Misri ni mbaya zaidi kuliko Hosni
Mubarak, dikteta wa nchi hiyo aliyeng’olewa madarakani. Akihutubia jamii
ya Wamisri waishio nchini Austria katika kongamano lililofanyika kwa
anuani isemayo:”Watetezi wa uhuru duniani wako dhidi ya mapinduzi ya
kijeshi”, Galloway amesema harakati za kimapinduzi nchini Misri
zitaushinda ufisadi ndani ya nchi hiyo akiwemo mgombea wa kiti cha urais
Abdel Fattah el Sisi.
Mbunge huyo wa Uingereza amesema, el Sisi ni
dikteta na kufafanua kwamba Abdel Fattah el Sisi ni mbaya zaidi kuliko
Hosni Mubarak, dikteta wa Misri aliyeng’olewa madarakani na anaungwa
mkono na Marekani na kupewa msukumo kwa utajiri wa baadhi ya nchi za
Kiarabu za Ghuba ya Uajemi. Galloway amemueleza el Sisi kuwa ni mabaki
ya utawala wa Mubarak na kutangaza uungaji mkono wake kwa wanamapinduzi
wote wa Misri katika mapambano dhidi ya el Sisi. Mbunge huyo wa
Uingereza aidha amesema tuhuma za mashtaka dhidi ya Muhammad Morsi, rais
wa Misri aliyeng’olewa madarakani ni za uwongo na hazina ukweli na
akalaani pia hatua ya kuitangaza harakati ya Ikhwanul Muslimin kuwa ni
kundi la kigaidi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment