Ndege za kijeshi za utawala haramu wa Israel kwa mara nyingine tena
zimekiuka anga ya Lebanon. Jeshi la Lebanon limetangaza katika taarifa
yake kwamba, ndege za kivita na za kijasusi za Israel zimepaa katika
anga ya Lebanon kusini mwa nchi hiyo na katika maeneo mengine ya nchi
hiyo. Taarifa ya jeshi la Lebanon imebainisha kwamba, hatua hiyo ya
jeshi la utawala haramu wa Israel, kwa mara nyingine tena imekiuka wazi
mamlaka ya kujitawala ya Lebanon na kupuuza pia azimio nambari 1701 la
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.
Serikali ya Lebanon imelaani
mara chungu nzima hatua za jeshi la Israel za kukiuka mara kwa mara anga
na mamlaka ya kujitawala nchi hiyo ya Kiarabu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment