Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema
kuwa, Tehran itaendelea na mazungumzo yake na kundi la 5+1 lakini wakati
huo huo itatoa majibu yanayofaa kwa vitendo vyote visivyo sahihi
vinavyofanywa na madola ya Magharibi.
Muhammad Javad Zarif amesema hayo leo katika ukurasa wake wa Facebook
na kusisitiza kuwa, Iran itaendelea na mazungumzo hayo kwa nguvu zake
zote na itatoa majibu yanayofaa kwa hatua yoyote isiyo sahihi
inayochukuliwa na dola lolote lile.
Ikumbukwe kuwa, siku ya Alkhamisi Wizara ya Hazina ya Marekani
iliyawekea vikwazo vipya mashirika na maafisa kadhaa wa Iran kwa madai
kuwa wamesaidia maendeleo ya nyuklia ya Iran.
Vikwazo hivyo vipya vya Marekani vimekuja licha ya Iran na kundi la
5+1 linaloundwa na nchi za Russia, China, Ufaransa, Uingereza, Marekani
pamoja na Ujerumaini kutiliana saini makubaliano ya nyuklia Novemba 24
mwaka huu mjini Geneva Uswisi ambayo kwa mujibu wake, pande zote
zilitakiwa kujenga hali ya kuaminiana na kurahisisha njia za utekelezaji
wa vipengee vya makubaliano hayo.
No comments:
Post a Comment