Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameeleza kuwa Jamhuri ya Kiislamu
ya Iran imedhamiria kufikia makubaliano kamili ya mwisho na kundi la
5+1. Muhammad Javad Zarif amesema Iran inafungamana na mchakato wa
mazungumzo hayo na kuongeza kuwa Tehran itaendelea na mazungumzo ya
nyuklia licha ya vizuizi vilivyojitokeza wiki iliyopita katika njia ya
mazungumzo ya nyuklia ya Iran na kundi la 5+1.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameyasema hayo katika mahojiano
aliyofanya na David Ignatius, mwandishi wa gazeti la Washington Post.
Washington Post limemnukuu Muhammad Javad Zarif na kuandika kuwa katika
makubaliano ya mwisho, Iran itathibitisha kwamba miradi yake ya nyuklia
inafanyika kwa malengo ya amani.
Wakati huo huo katika mahojiano yake na kanali ya CBS, Waziri wa
Mambo ya Nje wa Iran amevitaja vikwazo vya hivi karibuni vya Marekani
dhidi ya shakhsiya kadhaa na makampuni ya Iran kuwa ni makosa makubwa na
kueleza kuwa, Tehran hata hivyo itaendelea kuheshimu makubaliano ya
muda iliyofikia na kundi la 5+1 kuhusu miradi yake ya kuzalisha nishati
ya nyuklia.
No comments:
Post a Comment