Ripoti iliyotolewa na Umoja wa Mataifa imesema kuwa Uturuki
imepeleka zaidi ya tani 47 za silaha ili kuwaunga mkono waasi
wanaopigana dhidi ya serikali ya Syria tangu mwezi Juni mwaka huu.
Ripoti hiyo imeeleza kuwa, mwezi Septemba pekee Uturuki iliwapelekea
waasi wa Syria idadi tofauti za bunduki, ambapo kiwango kikubwa zaidi
kilikaribia tani 29.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki Levent
Gumrukcu awali alikanusha takwimu hizo lakini baadaye alikubali akidai
kwamba ripoti hiyo ya Umoja wa Mataifa ni kwa mujibu wa rekodi za
zamani. Urutuki ni miongoni mwa nchi zinazolaumiwa kuchochea mapigano
nchini Syria.
Katika upande mwingine zaidi ya waasi 100 wameuawa katika operesheni
ya anga iliyofanywa na jeshi la serikali ya Syria dhidi ya eneo
linalodhibitiwa na makundi ya waasi huko Aleppo kaskazini magharibi mwa
nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment