Muungano wa kitaifa wa kuunga mkono utawala wa kisheria nchini
Misri umetoa wito wa kufanyika maandamano ya mamilioni ya watu kupinga
serikali ya kijeshi.
Katika taarifa yake iliyotoa leo, sambamba na kusifu muqawama wa
wanafunzi wa vyuo vikuu vya Misri katika kukabiliana na serikali ya
kijeshi, muungan huo umelaani mashambulizi ya kinyama ya wanajeshi
watiifu kwa wafanya mapinduzi dhidi ya vyuo vikuu na kuwakandamiza
waandamanaji.
Muungano huo umewataka Wamisri kujitokeza kuandamana kwa
mamilioni kesho Jumanne na kusisitiza kuwa, jinai zinazofanywa na
serikali ya mpito ya Cairo hazitafumbiwa macho.
Hayo yanajiri huku serikali ya Misri ikiimarisha usalama katika
Medani ya Tahriri mjini Cairo na vikosi vya usalama na magari ya jeshi
yanafanya doria mjini humo. Taarifa zinasema kuwa baada ya kutolewa wito
wa maandamano ya kupinga jeshi, usalama umeimarishwa kwenye majengo ya
serikali na kwamba idadi kubwa ya askari na magari ya jeshi yamepelekwa
kwenye maeneo mbalimbali ya mji mkuu, Cairo.
No comments:
Post a Comment