Watu wanane wameuawa katika mlipuko uliotokea leo huko Mogadishu mji mkuu wa Somalia.
Watu wanane wamefariki dunia baada kuripuka bomu linaloongozwa
kutokea mbali. Bomu hilo lililipuka mapema leo kwenye mgahawa mmoja huko
Mogadishu mji mkuu wa Somalia.
Qadir Muhammad afisa polisi wa Somalia ameripoti kuwa wanajeshi
watatu pia wameuawa katika mripuko huo na hadi sasa hakuna kundi au mtu
aliyetangaza kuhusika na shambulizi hilo.
Afisa huyo wa polisi ya
Somalia ameongeza kuwa wanalishuku kundi la ash-Shabab kuwa limehusika
katika mripuko huo huko Mogadishu.
Kundi la wanamgambo wa ash-Shabab linadhibiti eneo kubwa la kusini na
katikati mwa Somalia na limekuwa likiendesha mashambulizi dhidi ya
vikosi vya serikali na wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Afrika
walioko Somalia.
No comments:
Post a Comment