Wapinzani wa serikali nchini Libya wametangaza kuwa wataendelea
kuzingira viwanda vya uzalishaji mafuta na bandari zake, kufuatia
kushindikana kufikiwa maelewano kati yao na serikali ya Tripoli. Mkuu wa
gadi ya usalama ya mzingiro katika bandari za Ra's Lanuf, As Sidr na az
Zaytuniyyah bwana Ibrahim Jadhran ametangaza kuwa, wapinzani
hawatozifungua tena bandari hizo za mafuta kwa kuwa serikali imeshindwa
kutekeleza masharti yao kabla ya kumaliza mzingiro huo.
Hii ni katika
hali ambayo kiongozi mmoja wa kamisheni ya nishati katika bunge la nchi
hiyo, ametangaza kuwa uzalishaji mafuta nchini Libya umepungua na
kufikia kiwango cha mapipa 100 kwa siku. Kabla ya hapo Waziri Mkuu wa
Libya Ali Zeidan alitangaza kuwa, kuna uwezekano wa kumalizika mzingiro
wa watu wenye silaha dhidi ya bandari za kusafirishia mafuta huko
mashariki mwa nchi hiyo. Ali Zeidan alisema kuwa, mzingiro huo uliodumu
kwa muda mrefu sasa ulitarajiwa kumalizika ifikapo jana Jumapili na
kuanza upya shughuli za usafirishaji mafuta.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment