Shirika la Msamaha Duniani (Amnesty International) limeutuhumu
utawala wa kifalme wa Bahrain kwamba, unawaadhibu na kuwatesa watoto
wanaoshikiliwa na utawala huo katika maandamano salama nchini humo.
Katika ripoti yake Amnesty International imesema kuwa, makumi ya watoto
wamekumbwa na vitendo vya kuteswa na kupigwa vikali na utawala wa
kifalme wa nchi hiyo tangu mwaka 2011.
Naibu Mkuu wa shirika hilo katika
eneo la Mashariki ya Kati na kaskazini mwa Afrika Said Mamdouh
ameutuhumu utawala huo wa Bahrain kwa vitendo hivyo vya kuwatesa watoto
na kutaka utawala huo uwajibishwe katika taasisi za kimataifa za kutetea
haki za binaadamu. Ameitaka serikali ya Manama kuwaachilia huru watoto
wote walio chini ya umri wa miaka 18 sanjari na kuitaka serikali hiyo ya
kidikteta kufanya uchunguzi kuhusiana na vitendo hivyo. Watoto
wasiopungua 110 walio na umri kati ya miaka 16 na 18 wanashikiliwa
katika jela za utawala wa Aal-Khalifa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment