Kwa akali Waislamu 23 wameuawa leo mjini Bangui mji mkuu wa
Jamhuri ya Afrika ya Kati, baada ya kushambuliwa wakiwa ndani ya
msikiti. Mauaji hayo yamefanywa na kundi la wanamgambo wa Kikristo la
Anti Balaka.
Sheikh Muhammad Wasil Imam wa Masjidul Noor mjini Bangui amesema
kuwa, Waislamu hao wameuawa baada ya kukimbilia Msikiti humo kwa lengo
la kujipatia hifadhi.
Sheikh Muhammad Wasil ameongeza kuwa, wanamgambo
hao wa Anti Balaka waliwauwa Waislamu hao kwa kuwakatakata na wengine
kuwachinja kama kuku kwa kutumia mundu. Imam wa Masjidul Noor ameongeza
kuwa, wanamgambo hao wa Kikristo hawakuwa na huruma hata kwa wanawake na
watoto, kwani wote waliokuwa wamejificha Msikitini humo waliuawa
kinyama na miili yao bado iko pambizoni mwa Msikiti huo. Ameongeza kuwa,
wahanga hao watazikwa pambizoni mwa Msikiti, baada ya majeshi ya nchi
hiyo kukataa kutoa ruhusa ya kuzikwa kwenye makaburi ya Waislamu
yaliyoko nje ya Bangui.
No comments:
Post a Comment