Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini amesema kuwa serikali yake
imezima jaribio la mapinduzi na kutangaza marufuku ya kutoka nje katika
mji mkuu Juba baada ya mapigano yaliyotokea usiku wa kuamkia leo kati ya
makundi hasimu ya jeshi.
Kiiri amewaambia waandishi habari mjini Juba hii leo kwamba jeshi la
Sudan Kusini limefanikiwa kuzima jaribio la mapinduzi na kusisitiza
kuwa, zama za mapinduzi ya kijeshi zimepitwa na wakati.
Machafuko hayo yameanza kufuatia wiki kadhaa za mivutano baada ya
Rais Kiir kumuuzulu makamu wake, Rick Machar mwezi Julai. Rais wa Sudan
Kusini amesema kuwa wanajeshi watiifu kwa Machar ndio waliosababisha
mapigano hayo. Ripoti zinasema kuwa, Machar amekamatwa na jeshi
limethibiti hali ya mambo.
Akitangaza marufuku hiyo Salva Kiir amesema kuwa, watu hawataruhusiwa
kutoka nje kuanzia saa 12 jioni hadi 12 asubuhi na kuwahakikishia
wananchi kwamba hali ya mambo ni shwari kwa sasa.
Salva Kiir na Rich Machar wanatoka katika makundi tofauti ya kikabila yaliyokuwa yakipigana huko nyuma.
No comments:
Post a Comment