Mahakama ya mjini Cairo nchini Misri imeanza vikao vya kuchunguza faili
la tuhuma zinazomkabili dikteta wa zamani wa nchi hiyo Hosni Mubarak,
wanawe wawili, waziri wa mambo ya ndani wa zamani, wasaidizi wengine
sita wa waziri wa mambo ya ndani na mfanyabiashara aliyetoroka nchi.
Habari zinasema kuwa, Mubarak na wanawe ambao ni Alaa na Gamal, Habib
el-Adly na wasaidizi wake sita na Hussein Salim mfanyabiashara
aliyekimbia wanatuhumiwa kwa kutekeleza mauaji dhidi ya waandamanaji
katika mapinduzi ya wananchi ya mwaka 2011 na kupora mali za umma. Kwa
mujibu wa habari SamiHafez Anan jenerali mkuu wa jeshi wa zamani nchini
humo leo atatoa ushahidi katika kikao cha siri cha mahakama dhidi ya
watuhumiwa hao. Siku ya Jumamosi, Mohamed Hussein Tantawi waziri wa
ulinzi wa zamani wa Misri, alitoa pia ushahidi kama huo. Kikao hicho cha
siku ya Jumamosi kilichofanyika kwa muda wa masaa manne, Tantawi
alijibu maswali 200 kutoka bodi ya mahakama na mengine 50 kutoka kwa
mawakili wa watuhumiwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment