Kikosi cha Operesheni cha Umoja wa Mataifa nchini Ivory Coast UNOCI
kimeitaka serikali ya Ivory Coast kuondoa kinga iliyoliwekea kundi la
Dozo ambalo lilitekeleza mauaji ya mamia ya wananchi wa nchi hiyo miaka
minne iliyopita. Taarifa iliyotolewa na UNOCI imeeleza kuwa, kundi la
Dozo limekuwa likikiuka mara kwa mara haki dhidi ya binadamu nchini humo
kwa kufanya mauaji na kuwanyonga watu nje ya vyombo vya mahakama,
kukamata watu wasio na hatia, wizi na utapeli.
Uchunguzi uliofanywa na
Umoja wa Mataifa unaonyesha kuwa kwa akali watu 228 wameuawa na wengine
164 kujeruhiwa kutoka mwaka 2009 hadi 2013 kutokana na mashambulio
yaliyofanywa na kundi hilo, katika hali ambayo kitengo cha haki za
binadamu cha UNOCI kinaamini kwamba idadi ya watu waliouawa ni kubwa
zaidi kuliko hiyo iliyotajwa. Umoja wa Mataifa umeitaka serikali ya
Ivory Coast ilidhibiti kundi la Dozo sanjari na kuchunguza jinai
zinazofanywa na kundi hilo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment