Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Saturday, December 7, 2013

Walioshambulia San'aa walikuwa raia wa Saudia

Jeshi la Yemen limesema kuwa, watu waliolishambulia jengo la Wizara ya Ulinzi ya nchi hiyo juzi Alhamisi walikuwa raia wa Saudi Arabia. Mkuu wa majeshi ya Yemenn amesema wakati wa kuwasilishwa ripoti ya awali kwa Rais Abd Rabbuh Mansur Hadi wa nchi hiyo hapo jana kwamba kulikuwa na wavamizi wasiopungua 12 walioshiriki kwenye shambulio la kigaidi katika jengo la Wizara ya Ulinzi ya Yemen na kuuwa watu 56. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, wavamizi hao wanaokadiriwa kwamba 12 walikuwa ni raia wa Saudi Arabia.
Kamati ya uchunguzi ya Wizara ya Ulinzi ya Yemen inaendelea kupokea taarifa mbalimbali kuhusu magaidi hao na malengo waliyokuwa wakiyafuatilia. Kundi moja la wanamgambo wenye uhusiano na mtandao wa al Qaida limekiri kuhusika na shambulizi hilo la kigaidi huko Sana'a.

No comments: