Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Thursday, November 21, 2013

Kony afanya mazungumzo na Rais wa CAR

Kiongozi wa waasi wa LRA wa Uganda Joseph Kony amefanya mazungumzo na rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati akiomba apewe msaada wa chakula na hifadhi huku akiendelea kusakwa na kikosi cha nchi kadhaa za Afrika.
Hayo yamedokezwa na mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa Abou Moussa ambaye amesema yamkini Kony ni mgonjwa na yuko hali mahututi.
Abou Moussa ameongeza kuwa alikutana na Rais Michel Djotodia wa Jamhuri ya Afrika ya Kati ambaye amemfahamisha kuwa amewasiliana na Kony.
Djotodia amesema Kony ameomba apewe magunia 20 ya chakula pamoja na hifadhi kwa ajili yake na wapiganaji wake katika Jamhuri ya Afrika ya Kati. Djotodia amesema hajui Konya yuko wapi lakini anaamini amejificha nchini humo. Abou Moussa amesema amemtaka Djotodia asimpe Konya chakula isipokuwa tu iwapo atajisalimisha.

Waasi wa Kikristo wa LRA wanaoongozwa na Kony wanatuhumiwa kuwaua takribani watu 100,000 katika miongo miwili ya ukatili wao huko kaskazini mwa Uganda.  Hivi sasa kikosi cha askari 3,000 wa Afrika kinachoongozwa na Uganda kinamsaka Kony, kikijumuisha pia askari wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Uganda, Sudan Kusini na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

No comments: