Askari mmoja wa utawala haramu wa Kizayuni ameuawa na vikosi vya Lebanon
baada ya kuvuka mpaka na kuingia katika ardhi za nchi hiyo. Tukio hilo
limetokea katika eneo la mpakani la Naqoura baada ya kuzuka mapigano
kati ya askari wa Lebanon na wa utawala wa Kizayuni na kupelekea
mwanajeshi mmoja wa Israel kuangamizwa. Kwa mujibu wa habari, askari
mwingine mmoja wa Lebanon ameuawa katika tukio hilo.
Vikosi vya jeshi la
Lebanon katika maeneo ya mpakani ya ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za
Palestina vimejiweka katika hali ya hatari huku jeshi la utawala haramu
wa Israel likiongeza idadi ya askari wake mpakani hapo. Tayari utawala
wa Kizayuni umekiri kutokea tukio hilo. Hili ni tukio la pili kujiri
ndani ya kipindi cha wiki mbili zilizopita kati ya pande mbili. Kwa mara
kadhaa utalawa haramu wa Kizayuni umekuwa ukikiuka anga ya Lebanon na
kuvamia ardhi za nchi hiyo mara kwa mara, huku jamii ya Kimataifa
ikinyamazia kimya vitendo hivyo vya kichokozi vya Israel.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment