Rais Michel Djotodia wa Jamhuri ya Afrika ya Kati
ameahidi kuwapa msamaha wanamgambo wa nchi hiyo endapo wataweka chini
silaha zao. Rais Djotodia ambaye nchi yake inakabiliwa na machafuko
ametangaza msimamo huo kama sehemu ya juhudi zake za kujaribu
kuhitimisha machafuko ya kikaumu na kidini yanayoikabili nchi hiyo.
Rais Djotodia amesema kuwa, wanamgambo wa Kikristo wa
Anti-Balaka wametuma ujumbe kwa serikali na kutangaza kwamba, wako
tayari kuweka chini silaha zao lakini wanahofia usalama wao. Amesema,
wanamgambo hao wametoa masharti ya kuweka chini silaha zao na mojawapo
ni kujumuishwa serikalini.
Rais Djotodia amesema kwamba, serikali yake iko tayari
kuwasamehe wanamgambo hao endapo wataaacha mapigano na kuweka chini
silaha. Wakati huo huo, hali ya kibinadamu katika mji mkuu wa Jamhuri ya
Afrika ya Kati, Bangui inaendelea kuripotiwa kuwa mbaya na baadhi ya
ripoti zinasema kuwa, mji huo unakaribia kukumbwa na maafa ya
kibinadamu.
No comments:
Post a Comment