Rais Omar Hassan al-Bashir wa Sudan ametangaza kuwa, anaunga mkono
juhudi za kurejesha amani na usalama katika jimbo la Darfur, magharibi
mwa nchi hiyo. Rais wa Sudan amesisitiza kwamba, serikali yake inaunga
mkono utekelezwaji wa makubaliano ya amani ya Doha Qatar kuhusiana na
usalama wa Darfur.
Rais al-Bashir amesema, serikali ya Khartoum inafungamana kikamilifu
na vipengee vyote vya makubaliano ya amani ya Doha, Qatar. Hayo yanajiri
katika hali ambayo, licha ya kuweko juhudi za kieneo na kimataifa za
kurejesha amani na uthabiti katika jimbo la Darfur, magharibi mwa Sudan,
eneo hilo limeendelea kushuhudia machafuko. Hivi karibuni watu 38
waliuawa katika mapigano ya kikabila kwenye mwa jimbo la Darfur,
magharibi Sudan jimbo hilo. Jimbo la Darfur la Sudan lina utajiri wa
mafuta, dhahabu na urani, suala linalolifanya eneo hilo kuwa kitovu cha
mapigano kati ya makundi ya waasi na jeshi la serikali ya Khartoum.
No comments:
Post a Comment