Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametoa wito wa kuweko kambi
iliyoungana kwa shabaha ya kupambana na ugaidi. Rais Hassan Rouhani
ametahadharisha kuhusiana na mashambulio ya kigaidi dhidi ya ulimwengu
wa Kiislamu na kusisitiza kwamba, kuna ulazima wa kuweko kambi moja
iliyoungana kwa ajili ya kupambana na ugaidi.
Rais Rouhani amesema hayo katika mazungumzo yake kwa njia ya simu na
Nouri al-Maliki, Waziri Mkuu wa Iraq na kubainisha kwamba, Iraq sio
mlengwa pekee wa mashambulio ya kigaidi bali vitendo hivyo vya kigaidi
vimeratibiwa ili kuzusha fitina na mifarakano katika ulimwengu wa
Kiislamu.
Kwa upande wake Nouri al-Maliki, Waziri Mkuu wa Iraq amesisitiza
katika mazungumzo yake na Rais wa Iran juu ya azma ya serikali yake ya
kupambana na ugaidi.Hayo yanaripotiwa katika hali ambayo, katika siku za
hivi karibuni, Iraq imeandamwa na wimbi jipya la mauaji na mashambulio
ya kigaidi.
No comments:
Post a Comment