Duru za habari nchini Saudia zinefichua kuwa, Bandar bin Sultan bin
Abdulaziz Al Saud Mkuu wa Shirika la Ujasusi la Saudi Arabia anapanga
njama za kumpindua Salman bin Abdulaziz Al Saud mrithi wa kiti cha
ufalme nchini humo. Habari zinaeleza kuwa, hivi karibuni Bandar alieneza
uvumi kwamba, mrithi huyo wa kiti cha mfalme hawezi kutekeleza majukumu
yake kutokana na kuelemewa na ugonjwa. Ripoti hizo zimeongeza kuwa,
Mkuu huyo wa Shirika la Ujasusi la Saudi Arabia ameanza mchakato wa
kufanya mazungumzo na mfalme wa Saudia kwa lengo la kutaka achaguliwe
mwana mfalme Muqrin bin Abdulaziz Al Saud au mtu mwingine ambaye ataweza
kutekeleza majukumu yake vizuri.
Nivyema kuashiria hapa kwamba Muqrin
alikuwa akishikilia nafasi ya Mkuu wa Shirika la Ujasusi la Saudi Arabia
kabla ya Bandar hajachaguliwa katika nafasi hiyo. kwa mujibu wa habari
banda anafanya njama hizo kwa lengo la kupanua satwa yake ya uongozi
nchini Saudia.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment