Social Icons

twitterfacebookgoogle pluslinkedinrss feedemail

Thursday, November 21, 2013

Zimbabwe yasisitiza kutaifisha migodi

Zimbabwe imesema haitalegeza msimamo wake wa kulazimisha mashirika ya kigeni yenye kumiliki migodi kuwauzia wazalendo weusi sehemu kubwa zaidi ya  hisa katika mashirika hayo.
Hayo yamedokezwa leo na Francis Nhema Waziri wa Vijana na Uwezeshaji wa Kiuchumi ambaye ameongeza kuwa mashirika ya uchimbaji migodi yatalazmika kuuza kwa uchache asilimia 51 ya hisa kwa wazalendo weusi huku benki zikitakiwa kuuza hadi asilimia 40 ya hisa kwa Wazimbabwe weusi.
Nhema amesema serikali haitalegeza msimamo wake na kwamba mashirika yanapaswa kuchukua hatua za kutekeleza sheria hiyo.
Serikali ya Rais Robert Mugabe imekuwa ikitekeleza sera ya kuhakikisha kuwa wazalendo weusi nchini Zimbabwe wanapata haki ya kumiliki mashamba, mashirika ya uchimbaji migodi na mashirika mengine ambayo kwa muda mrefu yamekuwa yakimilikiwa na wazungu waliowachache ambao walinyakua mali hizo wakati wa ukoloni.
Wafanyakazi wakiwa katika Migodi

No comments: