Jamii ya watu weusi nchini Marekani imelaani hukumu iliyotolewa na jopo
la majaji kuhusu kesi ya mauaji dhidi ya George Zimmerman. Zimmerman
alikuwa anakabiliwa na mashtaka ya kumuua Trayvon Martin, Mmarekani
mweusi mwenye umri wa miaka 17. Jopo hilo la majaji limetoa uamuzi huo
leo alfajiri kwa saa za hapa Tehran ambapo limesema Zimmerman hana hatia
na kwamba uchunguzi unaonyesha hakuhusika na mauaji hayo.
Wazazi wa
Travyon wamesema wanamuachia Mungu hayo yote na kusisitiza kwamba
hawajaridhishwa na uamuzi huo. Wamarekani weusi wamesema uamuzi wa jopo
hilo unairudisha nchi katika zama za ubaguzi wa rangi na wameitaka
mahakama ya kilele ya Marekani kuingilia kati suala hilo. Maandamano
yameripotiwa katika maeneo kadhaa ya Francisco huku waandamanaji
wakibeba mabango yenye jumbe za kulaani uamuzi huo. Baadhi ya mabango
yalikuwa na maandishi yanayosema: "Mfumo mzima ni wa kibaguzi" "Wananchi
tunasema Zimmerman ni muuaji"
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment