Mapigano makali yamejiri kati ya vikosi vya jeshi la Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo na kundi la wanamgambo huko mashariki mwa nchi
hiyo. Wakazi wa eneo la Nyamilima la mashariki mwa mkoa wa Kivu Kusini
wamesema kuwa, vikosi vya jeshi la Kongo vimeshiriki katika mapigano
makali na watu hao waliokuwa na silaha waliowataja kuwa wanamgambo wa
Mai Mai.
Mapigano hayo yalitokea jana Jumamosi huko mashariki mwa Kongo.
Wanajeshi wa Kongo waliamua kuwashambulia wanamgambo wa Mai Mai baada
ya kutiwa mbaroni kiongozi wao na baada ya jeshi la Kongo kuchoshwa na
vitisho vya mara kwa mara vya wanamgambo hao. Jeshi la Kongo limesema
limefanikiwa kuwafukuza wanamgambo wa Mai Mai huko Nyamilima na kwamba
oparesheni zao dhidi ya wanamgambo hao zitaendelea.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment