Watu wasiopungua 54 wameuawa katika mapigano makali ya kikabila yaliyotokea katika mji wa N'Zerekore nchini Guinea Conakry.
Duru za habari zinasema kuwa mapigano hayo yalianza baada ya watu wa
kabila la Guerze kumpiga na kumuua kijana mmoja wa ukoo wa Konianke kwa
tuhuma za wizi. Watu walioshuhudia wamesema baadhi ya wahanga wa
machafuko
hayo ya siku tatu waliuawa kwa kukatwa mapanga au kwa kuchomwa
moto wakiwa hai. Watu wengine zaidi ya 130 wamejeruhiwa katika
machafuko hayo.
Vikosi vya usalama vimelekwa katika eneo hilo la kusini mashariki mwa
Guinea na amri ya kutotoka nje imeanza kutekelezwa katika mji wa
N'Zerekore ambao ni wa pili kwa ukubwa nchini Guinea.
No comments:
Post a Comment