Mahakama moja ya mjini Abidjan imesikiliza kesi ya wapambe 84 wa karibu
wa rais wa zamani wa nchi hiyo Laurent Gbagbo. Miongoni mwa watuhumiwa
hao ambao hadi sasa wanaendelea kushikiliwa katika jela za Kodivaa ni
pamoja na Simone Gbagbo, mke wa rais huyo wa zamani na Michel Gbagbo
mtoto wa kiume wa Gbagbo.
Watu hao wanatuhumiwa kutenda jinai za
makusudi za kuhujumu uchumi, jinai za kivita, kuzusha machafuko katika
jamii na kushirikiana na magenge ya watu wenye silaha kwa lengo la
kuiangusha serikali ya hivi sasa nchini humo. Aidha mwendesha mashtaka
amewasomea mashataka watu wengine wanane kwa kutenda jinai ya mauaji ya
kizazi. Weledi wengi wa masuala ya kisiasa wameitaja hatua hiyo
iliyochukuliwa na mahakama kuwa haikutazamiwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment