Shirika la Kimataifa la Msamaha Duniani Amnesty International,
limevionya vikosi vya usalama nchini Zimbabwe, kutokana na ukandamizaji
dhidi ya wanaharakati wa haki za binaadamu na wapinzani wa serikali
nchini humo. Mratibu wa mipango ya shirika hilo barani Afrika Bwana Noel
Kututwa amesema kuwa, hatua zinazochukuliwa na vikosi vya usalama vya
Zimbabwe zinatia wasiwasi mkubwa kuhusu hatari ya kufanyika uchaguzi
mkuu katika hali ya ukandamizaji mkubwa dhidi ya wanaharakati wa haki za
binaadamu na wapinzani wa serikali ya Zimbabwe.
Kututwa amewataka
askari usalama nchini humo kuheshimu haki ya kujieleza. Uchaguzi mkuu
nchini Zimbabwe unatazamiwa kufanyika tarehe 31 mwezi huu. Katika ripoti
yake ya kurasa 63, Amnesty International yenye makao yake mjini London,
Uingereza, ilitangaza kuwa, pamoja na kupungua vitendo vya ukandamizaji
wa polisi nchini Zimbabwe ikilinganishwa na wakati wa uchaguzi
uliopita, lakini bado wanaharakati wa haki za binaadamu na wapinzani
nchini humo wanasumbuliwa na hali mbaya ya ukandamizaji.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment