Waziri wa Mambo ya Nje wa Venezuela, ElíasJosé Jaua, amesema kuwa, hadi
sasa afisa wa zamani wa Shirika la kijasusi la Marekani CIA, Bw. Edward
Snowden hajatoa majibu juu ya pendekezo la nchi hiyo la kumpa hifadhi.
Elíasamesema, serikali ya Caracas haina mawasiliano na afisa huyo wa
kijasusi wa Marekani.
Waziri huyo wa Mashauri ya Kigeni wa Venezuela
ameyasema hayo alipokuwa akijibu swali lililotaka kujuwa kama serikali
yake imepata majibu kutoka kwa Snowden baada ya Rais Nicolás Maduro wa
nchi hiyo kutangaza kumpatia hifadhi afisa huyo wa zamani wa CIA. Ijumaa
iliyopita rais wa Venezuela alitoa pendekezo la kumpatia hifadhi ya
urafiki Snowden. Venezuela ilichukua hatua hiyo kwa kile ilichosema kuwa
ni kuzuia kuhukumiwa afisa huyo kinyume cha sheria katika vyombo vya
sheria vya Marekani.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment