Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limesisitizia udharura wa kuongezwa idadi ya vikosi vyake nchini Sudan Kusini.
Baraza hilo limefikia uamuzi huo katika kikao maalumu kilichofanyika
kwa madhumuni ya kurefushwa kazi za askari wa kulinda amani wa Umoja wa
Mataifa katika nchi kadhaa duniani ikiwemo Sudan Kusini na kusisitizwa
juu ya udharura wa kutumwa vikosi zaidi katika maeneo ya mapigano,
likiwemo eneo la Jonglei huko Sudan Kusini.
Mapigano katika jimbo hilo kati ya jeshi la Sudan Kusini na makundi
ya wabeba silaha, yamepelekea makumi ya maelfu ya raia kuwa wakimbizi na
wengine kuuawa wakiwemo askari watano wa kulinda amani wa Umoja wa
Mataifa.
No comments:
Post a Comment