Watu wenye hasira wameandamana kote nchini Marekani
kulaani uamuzi wa mahakama moja nchini humo wa kumuondoa hatiani George
Zimmerman aliyemuua kijana Mmarekani-Mwafrika.
Maandamano makubwa yameripotiwa kufanyika huko Oakland,
California, Los Angeles, New York, Boston na San Francisco.
Machafuko
Marekani yalianza Jumamosi baada ya mahakama moja ya Florida kumuondoa
hatiani mlinzi Zimmerman ambaye alimuua kijana Mmarekani-Mwafrika
Trayvon Martin ambaye hakuwa na silaha.
Waandamanaji walibeba mabango yaliyokuwa na maandishi kama vile 'Tunataka Uadilifu' na 'Komesheni Ubaguzi'.
Duru zinaarifu kuwa idadi kubwa ya watu wametiwa mbaroni
huku polisi wakionekana kutumia mabavu dhidi ya waandamanaji. Wamarekani
wenye hasira wamekaidi ombi la rais Barack Obama ambaye amewataka
watulie na waheshimu uamuzi wa mahakamana.
No comments:
Post a Comment