Rais Michel Djotodia wa Jamhuri ya Afrika ya Kati amesema, rais wa
zamani wa nchi hiyo aliyeondolewa madarakani katika mapinduzi ya mwezi
Machi mwaka huu sasa anaweza kurejea nchini humo. Akiwa ziarani nchini
Benin, Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati amesema kuwa, Francois Bozize
ni raia wa Jamhuri ya Afrika ya Kati kwa hivyo anaweza kurejea nchini
kwake na kwamba wao hawapingi jambo hilo.
Mwezi Mei mwaka huu viongozi
wa Jamhuri ya Afrika ya Kati walitoa waranti wa kutiwa mbaroni Bozize
wakimtuhumu kutenda jinai dhidi ya binadamu na kuchochea mauaji ya
kimbari nchini humo. Hata hivyo rais wa hivi sasa wa Jamhuri ya Afrika
ya Kati hakusema iwapo Francois Bozize atatiwa nguvuni atakaporejea
nchini humo au la. Baada ya kupinduliwa, Bozize alikimbilia nchini
Cameroon, lakini sasa hajulikani aliko.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment