Duru za habari kutoka Ufaransa zinaarifu kuwa, Rais Abdelaziz Bouteflika
wa Algeria amerejea nchini kwake baada ya kupata matibabu nchini
Ufaransa. Habari zinasema kuwa, Rais Bouteflika ameondoka nchini
Ufaransa majira ya adhuhuri ya leo kuelekea nchini kwake. Rais huyo
mwenye umri wa miaka 76 alipelekwa nchini Ufaransa baada ya kukumbwa na
ugonjwa wa kiharusi mwishoni wa mwezi Februari ambapo awali alilazwa
katika hospitali ya kijeshi ya Valde Grace na kupelekwa katika hospitali
nyingine ya mjini Paris, Ufaransa.
Kukosekana kwake kisiasa nchini
Algeria, kuliibua maswali mengi hasa kuhusiana na nafasi ya uraisi
nchini humo. Hali hiyo ilivifanya vyama na makundi ya kisiasa
yanayoipinga serikali inayoongozwa na Rais Abdelaziz Bouteflika wa
Algeria, vilitaka kufanyika uchaguzi wa kabla ya wakati kwa mujibu wa
katiba ya nchi hiyo kutokana na kuugua rais huyo. Hii ni katika hali
ambayo hivi karibuni Rais huyo alitoa msamaha kwa maelfu ya wafungwa wa
nchi yake, kwa mnasaba wa kuwadia sherehe za kumbukumbu za uhuru wa nchi
hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment