Serikali ya Tanzania, imeionya Rwanda isijaribu kuishambulia kijeshi
nchi hiyo, vinginevyo itajibu uchokozi wowote ule kwa nguvu zake zote.
Kauli hiyo nzito ilitolewa jana na Wizara ya Mambo ya Nje ya Ushirikiano
wa Kimataifa ya Tanzania kufuatia matamshi makali yanayodaiwa kutolewa
na Rais Paul Kagame wa Rwanda, dhidi ya Rais Jakaya Kikwete na kutishia
kuishambulia Tanzania.
Msemaji wa wizara hiyo, Mkumbwa Ally, alisema
ingawa Serikali ya Tanzania hadi sasa haijawahi kuwa na ugomvi wa aina
yoyote ile na Rwanda, lakini amekiri kuwepo kile alichokiita kuwa ni
'kupishana lugha' baina ya Rais Jakaya Kikwete na Paul Kagame. Aidha
Mkumbwa alisema kuwa Serikali ya Tanzania ina ushahidi wa maneno
yanayodaiwa kutolewa na Rais Kagame katika moja ya hotuba zake
alizozitoa tarehe 30 Juni, nchini Rwanda. Kwa mujibu wa maneno hayo,
Kagame anadaiwa kutoa matamshi ya vitisho dhidi ya Rais Kikwete kwamba
anamsubiri katika wakati aujuao yeye ili amchape. Hii ni katika hali
ambayo mbali na Kagame, viongozi kadhaa wa Rwanda wamekuwa wakitoa kauli
za kejeli dhidi ya Rais Kikwete wa Tanzania. Hata hivyo Msemaji huyo wa
Wizara ya Mambo ya Nje ya Tanzania alisema, msimamo wa Tanzania uko
pale pale kwa kuitaka serikali ya Kigali ikubali kukaa meza moja na
wapinzani wake, ili kumaliza migogoro inayoendelea katika nchi hizo za
maziwa makuu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment