Leo ni Ijumaa tarehe 3 Ramadhani 1434 Hijria inayosadifiana na tarehe 12 Julai 2013.
Siku kama ya leo miaka 7 iliyopita Jeshi la utawala wa Kizayuni wa
Israel kwa mara nyingine tena lilifanya mashambulizi ya anga na bahari
huko Lebanon. Utawala wa Kizayuni ulifanya mashambulizi hayo kwa
kisingizio cha kukamatwa mateka wanajeshi wake wawili na wapiganaji wa
Harakati ya Hizbullah ya Lebanon kupitia oparesheni yake ya kujilinda.
Tel Aviv ilifanya mashambulizi hayo ya kijeshi huko Lebanon iliungwa
mkono na Washington lengo lake kuu likiwa ni kuvunja uwezo wa kijeshi wa
Hizbullah na kuipokonya silaha harakati hiyo inayohesabiwa kuwa nguvu
kuu ya mapambano huko Lebanon mbele ya jeshi ghasibu la utawala wa
Kizayuni.
Miaka 67 iliyopita katika siku inayosadifiana na hii ya leo hoteli ya
Mfalme Daud huko Baitul Muqaddas iliripuliwa kwa bomu na kundi la
Kizayuni la Irgun. Hoteli hiyo ilikuwa ikitumiwa sana na raia wa
Palestina na vilevile ikitumiwa kama mahali pa kufikia wageni. Kwa
kadiri kwamba bomu lililokuwa limetegwa ndani ya hoteli hiyo liliripuka
na kuuawa watu zaidi ya 200. Kuweko Wayahudi watano miongoni mwa
waliouawa katika mlipuko huo kunabainisha wazi namna Wazayuni
wasivyothamini hata maisha ya Wayahudi ili kutimiza malengo yao ya
kujitanua na kuzusha hofu miongoni mwa Wapalestina.
Na kwa mara ya kwanza katika historia ya mapambano ya ukombozi ya Waislamu, katika siku kama ya leo Tariq bin Ziyad aliwasili Uhispania akiwa na jeshi kubwa. Ushindi huo ulikuwa mwanzo wa kusonga mbele jeshi la Kiislamu huko Ulaya, ushindi ambao uliendelea hadi Ufaransa ya leo. Tariq bin Ziyad aliwasili Uhispania baada ya kuvuka mlango bahari kati ya Morocco na Uhispania unaojulikana kwa jina lake mwenyewe yaani "Jabal Tariq." Mlango bahari huo unatumika kama njia ya mawasiliano kati ya Bahari za Atlantic na Mediterania. Waislamu walitawala kwa karne nane huko Uhispania na kueneza mafunzo na utamaduni wa Kiislamu barani Ulaya baada ya kukombolewa Andalusia, moja ya sehemu ya Uhispania.

No comments:
Post a Comment