Kwa mara nyingine serikali ya Sudan imesisitiza kuwa, taifa la Misri
linaweza kumaliza lenyewe mgogoro ulioikumba nchi hiyo hivi sasa. Hayo
yamesemwa na Naibu Spika wa bunge la Sudan Samiya Ahmad Muhammad
alipokuwa akiongea na waandishi wa habari katika ofisi za bunge na
kufafanua kuwa, taifa la Misri linaweza lenyewe kumaliza mgogoro wa nchi
hiyo ili kwa mara nyingine taifa hilo muhimu liweze
kutoa mchango wake
chanya katika ulimwengu wa Kiarabu na Kiislamu na duniani kiujumla.
Aidha ameashiria kwamba, matatizo ya Misri ni ya ndani na kusisitiza
kuwa, serikali ya Khartoum huwa haiingilii masuala ya ndani ya nchi
yoyote duniani. Kwa upande mwingine Naibu Spika wa Bunge la Sudan
amesisitizia kuwepo uhusiano mwema baina ya nchi yake na mataifa
mbalimbali ya dunia. Hii ni katika hali hali ambayo mamia ya Watunisia
kwa mara nyingine leo wamefanya maandamano kumuunga mkono rais
aliyeenguliwa madarakani Muhammad Mursi wa Misri. Waandamanaji hao
waliokuwa na picha za Mursi, walitoa nara za kulaani hatua ya jeshi la
Misri ya kuingilia masuala ya siasa nchini humo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment