Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC, Bi. Fatou
Bensouda, ameondoa mashahidi watatu kwenye kesi ya jinai dhidi ya
binadamu inayomkabili Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya. Bensouda amesema
mashahidi wawili wamesisitiza kwamba hawawezi kuendelea kuwa mashahidi
kwenye kesi hiyo kutokana na kuhofia usalama wao.
Amesema pia kuwa,
ametathmini ushahidi wa shahidi mwengine na ameona hauna umuhimu mkubwa
na kwa mantiki hiyo ameamua kumuondoa. Itakumbukwa kuwa mahakama hiyo ya
ICC majuma kadhaa yaliyopita iliamua kwamba, Makamu wa Rais wa Kenya,
William Ruto atahudhuria tu vikao muhimu vya kesi yake mjini Hague na
kisha kushiriki kwenye vikao vya kawaida kwa njia ya video. Wachambuzi
wa masuala ya kisheria wanasema hatua hiyo ina maana kwamba kesi dhidi
ya Rais Kenyatta na Makamu wake zinaendelea kuwa dhaifu na huenda
wakafutiwa mashtaka iwapo matukio kama hayo yataendelea kushuhudiwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment