Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Abbas Araqchi, amekaribisha
matamshi ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza, William Hague ambaye
amesema nchi yake iko tayari kuimarisha uhusiano na Iran hatua kwa
hatua. Bw. Araqchi amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iko tayari
kuimarisha uhusiano na nchi zote za Ulaya ikiwemo
Uingereza ilimradi
uhusiano huo uwe wa kimantiki na unaoheshimu maslahi ya pande mbili.
Kauli ya Msemaji wa Wizara ya Mambo ya nje ya Iran inakwenda sanjari na
yale ya rais mteule, Dk Hassan Rohani ambaye amekariri mara kadhaa
kwamba sera za nje za serikali yake zitalenga kuimarisha uhusiano na
nchi zote duniani. Rohani amekuwa akisisitiza kwamba dunia inahitaji
mchango wa kila nchi ili mambo yawe shwari. Hata hivyo, Sheikh Hassan
Rohani amesema uhusiano wowote ule lazima ujengeke juu ya misingi ya
uadilifu na kuheshimiana.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment