Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia imesema kuwa jamii ya kimataifa ina
hamu kubwa ya kufanya mazungumzo na serikali ijayo ya Jamhuri ya
Kiislamu ya Iran kuhusu kadhia yake ya nyuklia. Taarifa hiyo imesema
kwamba, hapo jana wanadiplomasia wa Marekani, Uingereza, Ufaransa na
Uchina walikubaliana kwa kwauli moja kuwa, duru mpya ya mazungumzo na
Iran inapaswa kuanza punde tu serikali mpya itakapoanza kazi baada ya
kuapishwa rais mteule, Dkt. Hassan Rohani.
Kauli kama hiyo pia ilitolewa
na Bi. Catherine Ashton, Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya hapo
jana ambapo alisema kundi la 5+1 linatarajia kuanza mazungumzo na Iran
ili kutatua suitafahamu iliyoko kuhusu kadhia yake ya nyuklia. Ashton
amesema kundi hilo linalojumuisha nchi 5 wanachama wa kudumu wa Baraza
la Usalama la Umoja wa Mataifa pamoja na Ujerumani lina matumaini kwamba
litaweza kufikia makubaliano muhimu na serikali ijayo ya Jamhuri ya
Kiislamu ya Iran.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment